Shairi na Misemo
0/5 - - 0 vote

02/13/2019 02/15/2019

TUJIKAZE KISABUNI TUIMARIKE MASOMONI                                                                                       

Enyi Ndugu wazalendo nahubiri hadharani

Tuzidi kukaza mwendo tuongoze shule yetu

Nidhamu iwe shuleni maendeleo yatazidi

Tujikaze kisabuni tuimarike masomoni

Shule yetu ni ajabu wanafunzi ni minane

Amani tunaiomba Maulana atulinde

Tupate alama zetu tuongoze nchi pia

Tujikaze kisabuni tuimarike masomoni

Tuwaheshimu walimu adabu tujifunze

Elimu tutaipata tutimize lengo letu

Tuwaheshimu kwelikweli wasije kututhulumu

Tujikaze kisabuni tuimarike masomoni

Walezi kajitolea wahakikishe tuwe shuleni

Mahitaji wametimiza tusome kwa bidii

Wamezunguka pembe zote wapate kulipa karo

Tujikaze kisabuni tuimarike msomoni

Napuliza vuvuzela kusema kwa ukaidi

Tusipoteze hela zao tukawavunja nyoyo zao

 Wahakikisha twala vyema nasi tuwafurahishe

Tujikaze kisabuni tuimarike masomoni

Sitaki   kunena sana nikapigwa marufuku

Asikiaye ana nafasi aweze kubadilika

Ninafunga kinywa changu niliyonena yametosha

Tujikaze kisabuni tuimarike masomoni

 By.....JANE KEMUNTO

Share this page

0 comment

0 star
+ =

Follow us

  • http://www.facebook.com/Elimu-Holdings-Limited-1538954733045502/?ref=br_rs
  • http://www.twitter.com/elimuholdings

2008-2020 © @elimuholdings